Ijumaa, 2 Aprili
Wakati mwingine tamaduni tofauti na lugha tofauti hufanya ujipate katika mambo yasiyo ya kawaida kwako. Kwa mfano:
Baada ya kurekodi filamu ya leo, nilienda nyumbani usiku. Nilipofika mlangoni, kulikuwa na watoto takriban ishirini wananingoja na wakaniita "ROSE, UMESHINDAJE?" Baada ya salamu tulikaa na wao na kuongea. Watoto wa vitongoji duni hucheza na kukimbia sana. Mtu moja aliyekuwa hapo alizunguka akiwa amebeba chupa kubwa. Nilimuuliza kwa nini anakibeba chupa hicho, alinieleza kwamba ni mbwa wake. Mwengine alikua anazunguka akijifanya yeye ni mwanajeshi. Alikua na bunduki ya plastiki mkononi. Watoto hawa hawana mengi lakini bado wanaweza kutumia mawazo yao ili kucheza na wenzao na inanipa msukumo kuona vitu kwa macho yao.
Jioni tuliangalia mechi kati ya Barcelona na Arsenal. Mechi ilikua ya kusisimua sana na nilifurahia kuiona na majirani wangu. Tuliku watu tisa tukitizama televisheni ndogo mno. Televisheni yenyewe haikuwa na sauti basi ikabidi tuweke redio ili tusikie mtangazaji akisimulia mechi kwa lugha ya Kiswahili.
Sikuwa naweza kuona chochote. Nilijaribu nione mpira ulipo lakini televisheni ilikua ndogo sana. Sikusema lolote lakini, niliendelea kutizama. Kuongezea hayo sikumuelewa mtangazaji kwa redio. Nilipiga nduru nilipoona timu ya Barcelona ikitingisha wavu. Wengine hawakufurahia hivyo maanake walikuwa mashabiki wa timu ya Arsenal.

Hata hivyo nilifurahia kuona mechi hiyo. Baada ya mechi kuisha, niliambiwa "Rose, mabao hayakuwa ishirini kwa Barcelona sawa!". Kesho kuna mechi ingine.












