November 2010

JUMAMOSI FEBRUARI 27


Leo ni siku kubwa kwangu. Ni siku yangu ya kwanza ndani ya nyumba ya Kiswahili. Katika vitongoji duni vya Mombasa, hhizi nyumba ndizo ziko nyingi. Hazina rangi, na zimejengwa na simiti na mabati, saa zigine hata na matope.
Unaingia nyumba kwa kupitia geti. Kwa sababu ya usalama, huwa kuna milango miwili au mitatu. Kila chumba kina mlango mmoja na dirisha moja. Kwa chumba hicho kidogo kunaa familia nzima. Vyumba hivi vya Kiswahili hushikilia watu hata ishirini ama thelathini. Choo na bafu ni moja na hutumiwa na kila mtu.


 

 

 

Ninakaa kwa chumba change nikingoja chakula - wali na mayai. Winston anashangazwa na jinsi nilivyotulia. Kichwa change kina mawazo mengi lakini Winston na Annette hawajui. Naogopa kwamba wakienda nitakuwa peke yangu. Kwamba itachukua mda kabla nizoeane na watu hapa. Lakini nikavumilia.


 

 

 

 

IJUMAA FEBRUARI 26


Jana niliamka nikihisi ugonjwa. Nilijaribu kuamka lakini nikalemewa nikarudi kitandani. Nilikua na shida ya tumbo. Baada ya masaa ya uchungu na kutapika, nikaamua niende hospitalini. Daktari alinipa madawa na nikarudi hotelini. Lakini nikaanza kupata jot ya mwili.
Siku ya leo ndio siku ilikua na joto zaidi, nyuzi 35 kwa kivuli. Bado sikujihisi mzima, lakini ilibidi kazi iendelee. Nilikua na furaha maanake nilikua nimenunua vitu nitahitaji nikiingia kwa nyumba yangu ya Kiswahili. Nitahamia huko kesho.



Nyumba yangu ya Kiswahili ni ndogo na ina wadudu, nzi na mbu. Itakua ngumu kuishi hapo. Kuelewa vizuri maisha yangu hapo lazma uone filamu yangu.
Huko Sweden watu wanajitayarisha kuenda kustarehe kwa vilabu na marafiki lakini hapa Kenya lazma tuchape kazi siku zote saba za wiki.


Mombasa ni jiji la pili kubwa nchini Kenya. Ni jiji lililo na bandari ya Kenya na huwa na watalii wengi. Watu wengi huku ni waislamu na watu wa asili ya kimijikenda. Mombasa ni jiji lenye joto na kuzuri sana. Watu wengi huvutiwa na mahala hapa.


Wakamba ni baadhi ya makabila waliokuja hap kufanya kazi ya uchongaji wa mbao. Wengi wao wameacha familia zao huko bara na wamekuja kufanya kazi mjini.
Tuliopfika Mombasa, nilishangazwa na joto iliopo hapa. Huko wamunyu hali ya anga ilikua ya baridi. Ilikua ni usiku lakin joto ilikua nyingi kupindukia, takriban nyuzi 30. Niliogopa kufikiria joto itakuaje mchana ukifika. Hata wakaazi wa hapa walikua wanalalamika ju ya joto.
Hoteli yetu ilikua katikati mwa mji wa Mombasa. Nilivyokaa ndani ya gari nilitamani upepo. Lakini baadaya kuingia hotelini nilipata kipepeo cha stima ambayo niliwakisha kwa haraka. Sisi tutakaa hapa hotelini lakini Rose atakaa chaani.


Jumatano Februari 24


Leo hii niliamka saa kumi na moja asubuhi. Tutachukua picha za Joshua na Julius wakitoka nyumbani kwao. Tutarekodi wakiagana na mambo yote yatakayotokea.
Baada ya masaa kumi kwa basi tuliwasili kwa hotelini. Tulikuwa wachovu, tumechoka na tuna njaa. Tulifurahia kutumia choo safi na bafu baada ya kutoka kwa kijiji ambacho hakikuwa na vitu hivi. Chumba kilikua na stima na pia nikapata nafasi ya kujiona kwa kioo kwa mara ya kwanza baada ya wiki nzima. Nilioga na kuingia kitandani nikishukuru kwa yote niliyonayo maana wengine hawana kama mimi.


Kuamka asubuhi nilihisi furaha kutumia choo safi. Nilikua na furaha nikijitayarisha kuenda kwa kitongoji duni kesho. Nitakua nikiishi kwa nyumba ya Kiswahili. Mpaka siku hiyo tutakua tunajitayarisha.
Wacha nikueleze majina yetu na kazi tunayoifanya:
Winston: ni mpigaji picha ya filamu. Huwa kila mara anatafuta vitu kwa mifuko yake. Lakini ni mcheshi, na mwenye kipawa ya kazi yake. Anapenda pia kuchekesha watu.
Rose: ni mwanahabari na kiongozi wa kikundi hii. Yeye huongea sana na hujadiliana na kila mtu. Yeye huwa na ubunifu, na mwenye kufanya kazi kwa dhati. Hupenda sana kusema "filamu yangu ifuatayo itakuwa ju ya...."

JUMANNE FEBRUARI 23


Tuliamka saa kumi na moja asubuhi. Tulikuwa katika shamba. Kulikuwa kunapendeza sana. Baada ya kiamsha kinywa tulirekodi watoto wakijiandaa kuenda shuleni. Tulienda nao hadi shuleni na kuendelea kurekdi wakiwa huko. Niliulizwa maswali na wanafunzi wengine juu ya maisha ng'ambo na kwanini tuna tengeneza filamu. Watoto hao walikua watiifu sana.
Ilipofika saa nne hivi tulishuhudia mbuzi akichinjwa. Tulishtuka sana na mimi na Winston tulisimama tumepigwa na bumbuwazi, tukisikia mlio wa mbuzi huyo. Hatukuwai kushuhudia kisa kama hicho. Jionee picha mwenyewe.


Baada ya Joshua na Nguguye kupanga bajeti ilikuwa wakati wa kuchoma mbuzi huyo.
Kulikuwa na joto kali. Nyama ya mbuzi ilikua ndani ya ndoo. Nzi wengi walizunguka nyama. Nyama zikawekwa ju ya jiko na kuchomwa. Joshua aliku mpishi akigeuza nyama kila upande. Alinipa kidogo nionje, nikaitafuna na kitu kilivunjika mdomoni. Mdomo wangu ulijaa ladha ya nyama na maini. Winston alikua bado katika hali ya mshtuko kwa kuona mbuzi akichinjwa. Si rahisi kuzoea vile wanatengeneza nyama lakini nilifurahi vile wao walifurahia.