JUMAPILI FEBRUARI 21
Leo imekua siku iliyozaa matunda mengi. Siku ambayo najihisi nimfanya kazi ya maana.
Asubuhi, tuliskiza hadithi ya Joshua kuhusu maisha yake ya utotoni.Hadithi ambayo ilikua tofauti na yangu ya Iran ama ya Winston ya New Zealand. Hadithi ya ukweli. Tulirekodi filamu kila mahali tulienda. Saa zingine tulichanganyikwa na kitu cha kuweka filamu maanake mabo yalikua mengi. Ilibidi tuchukue kila kitu maanake wakati mwingine vitu vidogo vidogo ndivyo hufanya filamu ikawa nzuri. Tulipanda piki mbili, watatu kwa kila moja, na kuenda kwa nyumba ya Julia ambayo ilikua kilomita 3 hivi na nyumba ya Joshua. Kukutana na Julia ilinifanya nione kwamba hata kama hawana mali nyingi, wamejaa na furaha na tabasamu kwa maisha yao.

Tuliongea na mamake Julia ambaye alitupa hisia na maoni yake mengi. Mwanamke wa miaka 90 na aliye na nguvu na furaha. Hadithi zake zilikua za kusisimua. Alikua mwanamke mwenye roho safi. Nahisi kama tumeendelea sana kama dunia lakini tumepoteza uanadamu wetu na badala yake ni chuki, tama, uwivu na mengineyo.

Nilipongea na bibi ya Julius nilipata kujua megi kuhusu maisha yao. Wamekua wakiishi kama bwana na bibi kwa miaka 13. Katika miaka hiyo yote wameshindwa kupata motto. Kwa Mary kupata motto itabidi atumie pesa nyingi na apate madawa mengi. Na pesa hiyo aliku hana kabsa.
Julius alitukaribisha chai kwa mkahawa moja. Baada ya chai tulipanda piki piki na kurudi nyumbani kwa Joshua. Jioni tukapika chakula cha join na bibi ya Joshua.
Sijui kwanini lakini huku kambiti nahisi njaa kila wakati. Labda ni kwasababu nala kiamsha kinywa na chakula cha join pekee yake.
Skriv en kommentar