Jumatatu Februari 22
Mada ya leo imehusu choo. Imekua shida kuenda haja kubwa, ktu ambacho sijatilia maanani huko nyumbani Sweden. Huko Sweden ni lazma tuanze keshimu choo. Baada ya siku nyingi, na mahojiano mengi Winston alitueleza tujaribu kuona choo hicho kama choo cha hoteli alafu tutaweza kuitumia.

Lakini kwa sasa ilibidi tupakie mitambo yetu na tuende jijini. Tukiwa njiani, nilihisi kuenda haja kubwa. Tulitafuta choo kwa muda lakini tukapata choo moja kando ya duka la fundi wa simu. Choo hicho kilikua kichafu kupindukia. Nilijaribu kuingia, lakini nikifika ndani nalemewa na harufu mpaka inanibidi nitoke. Nilianza kulia na Winston akaanza kunicheka.
Tukirudi nyumbani kwa Joshua, tulipanga na Annette vile ataenda kutumia choo cha Joshua. Baada ya kula chakula cha jioni cha maharagwe, Annette alilazimika kutumia choo. Akajiamii na taa na manukato na akaenda chooni. Shida ya harufu ilitatuliwa.

Kesho kutakua na shughuli nyingi. Lazima tuamke mapema kupiga filamu ya jua ikipaa, halafu niwatengenezee watoto chai ili waende shule. Alafu tutaona mbuzi akichinjwa.
Skriv en kommentar