Ijumaa, 2 Aprili


Wakati mwingine tamaduni tofauti na lugha tofauti hufanya ujipate katika mambo yasiyo ya kawaida kwako. Kwa mfano:


Baada ya kurekodi filamu ya leo, nilienda nyumbani usiku. Nilipofika mlangoni, kulikuwa na watoto takriban ishirini wananingoja na wakaniita "ROSE, UMESHINDAJE?" Baada ya salamu tulikaa na wao na kuongea. Watoto wa vitongoji duni hucheza na kukimbia sana. Mtu moja aliyekuwa hapo alizunguka akiwa amebeba chupa kubwa. Nilimuuliza kwa nini anakibeba chupa hicho, alinieleza kwamba ni mbwa wake. Mwengine alikua anazunguka akijifanya yeye ni mwanajeshi. Alikua na bunduki ya plastiki mkononi. Watoto hawa hawana mengi lakini bado wanaweza kutumia mawazo yao ili kucheza na wenzao na inanipa msukumo kuona vitu kwa macho yao.
Jioni tuliangalia mechi kati ya Barcelona na Arsenal. Mechi ilikua ya kusisimua sana na nilifurahia kuiona na majirani wangu. Tuliku watu tisa tukitizama televisheni ndogo mno. Televisheni yenyewe haikuwa na sauti basi ikabidi tuweke redio ili tusikie mtangazaji akisimulia mechi kwa lugha ya Kiswahili.


Sikuwa naweza kuona chochote. Nilijaribu nione mpira ulipo lakini televisheni ilikua ndogo sana. Sikusema lolote lakini, niliendelea kutizama. Kuongezea hayo sikumuelewa mtangazaji kwa redio. Nilipiga nduru nilipoona timu ya Barcelona ikitingisha wavu. Wengine hawakufurahia hivyo maanake walikuwa mashabiki wa timu ya Arsenal.



Hata hivyo nilifurahia kuona mechi hiyo. Baada ya mechi kuisha, niliambiwa "Rose, mabao hayakuwa ishirini kwa Barcelona sawa!". Kesho kuna mechi ingine.


Jumanne, 30 Machi


Kwa vile Winston ameenda, nitaendelea kuchukua picha kwa niaba yake. Sababu ya mimi kukaa ni kwasababu tunahitaji kurekodi picha zaidi za filamu yangu. Bado sijui nitachukua mda gani huku.


 

 

 

 

 

Jumatatu, 29 Machi



Ilikua wakati wa Annette na Winston kutoka Kenya na Kurudi nyumbani. Walipoondoka nilihisi upweke mwingi sana, nilikua pekee yangu.


Nitamalizia mikutano kadhaa Nairobi alafu nirudi Mombasa kama saa saba mchana. Kila kitu nilikua nafanya kilichukua mda mrefu kuliko vile nilitarajia. Niliwachwa na basi, gari la moshi na hata ndege. Nilipokumbuka vile kulitendeka kwa basi siku chache zilizopita, singesafiri na basi ya usiku. Niliamua kukodisha teksi inifikishe Mombasa. Safari ilikua mbaya sana. Dereva alipeleka teksi kwa kasi sana, na hata wakati mwingine karibu asababishe ajali mbaya. Lakini kwa majaliwa ya mwenyezi mungu niliwasili Mombasa vyema. Nilienda hotelini nimechoka na nikiwa na njaa mno.
Nilikaa wikendi hio kwa hoteli nikingoja Joshua arudi kutoka Nairobi.



Nilipokua Mombasa, tulionana na Ken. Ken alinionyesha Mombasa kwa njia tofauti na vile nilikusudia. Ken ni mtu mzuri mwenye roho nzuri ya kusaidia watu. Yeye husaidia vijana wa mtaa wake, na akaanzisha timu ya kandanda inayoitwa Krack United (www.krackunited.com). Watoto wa timu hiyo ni wachezaji mpira wazuri sana na nilipata bafasi ya kuwapiga picha wakicheza mpira. Amenifundisha mengi.


 

 

Alhamisi, 25 Machi


Nasikitika kusimamisha taarifa ya safari yetu kutoka Masai Mara hadi Nairobi. Jambo hili ni muhimu.
Katika wiki sita tulizokua hapa Kenya nimejaribu kupata nafasi ya kumuona makamu wa rais. Kwa wale wasiojua, kura za mwaka wa 2007 ulizua zogo nchini Kenya hadi watu takriban 1000 walikufa na karibu watu 500,000 wliondolewa manyumbani mwao. Ili kusimamisha vita hivi, makamu wa rais na rais walikubali kugawa mamlaka na waziri mkuu.
Nimejaribu kuonana na makamu wa rais kwa njia zote. Nimepiga simu ofisini mwake kila siku na msaidizi wake hunuambia kila mara kwamba hana nafasi kwa sasa. Lakini sikufa moyo, niliamua kwamba lazima nitamuona.


Wiki iliyopita, msaidizi wake alinijulisha kwamba tutapata nafasi ya kuhojiana na makamu wa rais jumanne tarehe 23 mwezi wa Machi saa tatu unusu asubuhi. Nilifurahi sana, Annette na Winston walitabasamu kwa furaha tele.


Siku ilipofika, tulijitayarisha vyema kabisa. Maswali tutauliza, kamera tukaiangalia kama iko sawa, kila kitu tulichobaini kuwa ni muhimu tulichunguza. Tukielekea kumouna makamu wa rais, simu ililia na msaidizi wake akatujulisha kwamba mahojiano yamegeuzwa kua saa kumi siku hiyo. Saa kumi ilipofika tulikuwa ofisini mwake. Chumba chenyewe kilikuwa kimeimarika sana. Lakini tulikosa kumuona siku hiyo maanake alikuwa hajatoka bunge bado. Tuliambiwa kwamba tutaelezwa kesho wakati ambayo atapatikana.
Tulirudi hotelini na huzuni sana. Siku ifuatayo nilipiga simu ofisini mwake kila wakati. Niliambiwa ameingia bunge tena. Ilipofika saa kumi, nilikua nimekufa moyo, ilikua imebaki siku hiyo tu kuhojiana na yeye kwa sababu Annette na Winston walikua wanarudi nyumbani siku ya Alhamisi. Nilikua na huzuni mwingi huku nikijaribu kufikiria njia zingine na kupata kuonana na makamu wa rais.


Mara simu ililia. Msaidizi wa makamu wa rais alikua kwa simu akiniambia nifike kwa ofisi mara moja saa hio. Hoteli ilikua kama dakika thelathini kutoka ofisi ya makamu wa rais. Msaidizi wake alisema niwe hapo kwa dakika kumi. Niliambia Annette na Winston, "Twendeni saa hii, TWENDENI".



Tuliingia teksi na kumwambia dereva aharakishe. Lakini njiani tukapata msongamano wa magari. Kulikuwa kuna nyesha na hatukuweza kutoka kwa gari. Niliuliza dereva kama angeweza kupeleka kwa bara bara iliyo kando yetu ya magari zilizokua zinaenda njia mbadala na sisi. Aliniangalia ni kama nimepagawa, huku Annette anamwambia afanye hivyo. Winston mwishowe akasema tutoke na tukimbie mpaka huko. Tulitoka na kuanza kukimbia ni kama sisi ni wenda wazimu. Lakini hatukujali manake ilikua muhimu sana tumuone makamu wa rais.
Tulifika kwa ofisi yake tumelowa maji, tukihema sana. Lakini tulikua na furaha tele kupata nafasi hii. Mahojiano yalikua mazuri na tulimshukuru makamu wa rais kwa nafasi hio.

Jumapili, 21 Machi


Askari wawili na bunduki walikuja kwa gari letu. Tuliongea na dereva wetu aongee nao kwasababu mwili wangu ulikua mchovu sana. Askari hao walitaka pesa ili kuturuhusu kuingia mahali hapo. Tulikua hatujabeba pesa zozote kwasababu tulikua tumezoea kulipa na kadi ya benki. Askari walituambia eti ni lazima turudi Nairobi tuchukue pesa halfu ndio turudi. Nilikasirika sana na tukaanza kubishana na askari hao. Mwishowe dereva wetu ndie aliongea nao na wakaturuhusu tuingie Masai Mara.


Masai Mara ni pahala pazuri mno. Wanyama ni wengi na wanazurura kila mahali. Jioni hiyo tulisherehekea kwa mvinyo na chakula.


Siku iliyopita niliozwa kwa dereva wetu wa kimasai. Tulipokua tunakula chakula cha jioni, alitaka kutumia wazazi wangu ng'ombe 40 na matandikio ya kitanda. Nilijaribu kumweleza kua sio lazma, Winston nae alikataa hivyo na akaiambia kua hivyo ndivyo inavyofaa.
Jumatatu saa kumi na moja tulirauka na kuanza safari yetu kuelekea Nairobi. Huko Nairobi tuko na mahojiano muhimu.