Wakati wa kuenda Kenya kutengeneza Filamu inakaribia. Kila kitu kinaenda vyema lakini mda unayoyoma.


Leo nimegundua kwamba mpigaji picha wangu hataweza kuja name Kenya. Nilishikwa na wasiwasi, na nikajaribu niwezavyo kutafuta mwengine. Bahati nzuri rafiki yangu mmoja akaniambia kuhusu mpiga picha mmoja anaitwa Winston, na hapo ndipo nimakjua.
Winston alizaliwa nchi ya New Zealand na amefanya kazi ya upigaji picha kwa muda mrefu. Alikuja Sweden kufuata mpenzi wake. Nilimpigia simu na tukaagana kukutana naye katika mkahawa. Tulipoonana nailimuuliza "ungependa kuenda name Kenya kwa mud wa wiki mbili tutengeneze filamu?"


Alishtuka kidogo lakini akanijibu "ndio". Akaagiza kahawa na tukaanza kufanya mipango. Lakini wakati mwengine najiuliza kama anaelewa vyema nilichomueleza tunaenda kufanya. Lakini ni sawa, wacha tufanye mipango. Tuonane Kenya!