Jumatatu, 29 Machi

Ilikua wakati wa Annette na Winston kutoka Kenya na Kurudi nyumbani. Walipoondoka nilihisi upweke mwingi sana, nilikua pekee yangu.
Nitamalizia mikutano kadhaa Nairobi alafu nirudi Mombasa kama saa saba mchana. Kila kitu nilikua nafanya kilichukua mda mrefu kuliko vile nilitarajia. Niliwachwa na basi, gari la moshi na hata ndege. Nilipokumbuka vile kulitendeka kwa basi siku chache zilizopita, singesafiri na basi ya usiku. Niliamua kukodisha teksi inifikishe Mombasa. Safari ilikua mbaya sana. Dereva alipeleka teksi kwa kasi sana, na hata wakati mwingine karibu asababishe ajali mbaya. Lakini kwa majaliwa ya mwenyezi mungu niliwasili Mombasa vyema. Nilienda hotelini nimechoka na nikiwa na njaa mno.
Nilikaa wikendi hio kwa hoteli nikingoja Joshua arudi kutoka Nairobi.

Nilipokua Mombasa, tulionana na Ken. Ken alinionyesha Mombasa kwa njia tofauti na vile nilikusudia. Ken ni mtu mzuri mwenye roho nzuri ya kusaidia watu. Yeye husaidia vijana wa mtaa wake, na akaanzisha timu ya kandanda inayoitwa Krack United (www.krackunited.com). Watoto wa timu hiyo ni wachezaji mpira wazuri sana na nilipata bafasi ya kuwapiga picha wakicheza mpira. Amenifundisha mengi.



Skriv en kommentar