Jumamosi, 20 Machi




Safari yote ya kuelekea Nairobi tulikua macho kama popo. Tulikua hatujalala kwa masaa 29 na hatujakula kwa masaa 16. Tulipokua tunaelekea Masai mara niliona kweli tumekuwa wavumilivu. Mlipuko wa risasi ulikua haututatizi tena. Ilitusumbua tu dakika kama thelathini baada ya kuusikia mlipuko huo. Katika safari hii tumekuwa mashujaa kama wanajeshi. Tulivumilia mengi na wakati ukizidi kuenda, na matukio yakiongezeka, tulizidi kua wavumilivu. Rafiki yangu mmoja wa dhati aliniandikia na kuniambia kwamba anaona safari hii imenibadilisha sana. Tumeona mengi hapa Kenya. Tumepata hisia nyingi tofauti ambayo hatukudhani yapo. Tunashukuru kwa yale ambayo tunayo. Nchi hii imetuathiri kwa njia nzuri. Kila siku ni kama miaka mengi. Nilianza kuogopa kurudi Sweden manake sikujua vile safari hii imeniathiri na vile watu nyumbani watanichukua.

 

 


Tukielekea Masai Mara: Jua ilikua kali zaidi tulihisi tuko jikoni. Miguu na migongo yetu ilikufa ganzi. Tulikua tumekaa kwa gari kwa mda wa masaa manne na hapakua na afasi ya kunyorosha miguu. Nilianza kupoteza uvumilivu wangu. Niliona kama hatutawahi kuhitimu lengo letu. Niliambia dereva asimame, nikafungua mlango wa gari na nikashuka. Sikufikiria nilichokua nafanya mpaka nilioanza kukumbuka mahali nilpokua. Kulikua na wanyama wa pori wengi kama chui na simba katika mahali hiyo. Pole pole nilirudi kwa gari na kuingia, huku nikishukuru kuwa ndani na si nje ya gari.



Masaa mawili baadaye tulifika kwa lango la Masai Mara. Askari wawili walitukujia.......mengi zaidi kesho.



Skriv en kommentar