Alhamisi, 25 Machi


Nasikitika kusimamisha taarifa ya safari yetu kutoka Masai Mara hadi Nairobi. Jambo hili ni muhimu.
Katika wiki sita tulizokua hapa Kenya nimejaribu kupata nafasi ya kumuona makamu wa rais. Kwa wale wasiojua, kura za mwaka wa 2007 ulizua zogo nchini Kenya hadi watu takriban 1000 walikufa na karibu watu 500,000 wliondolewa manyumbani mwao. Ili kusimamisha vita hivi, makamu wa rais na rais walikubali kugawa mamlaka na waziri mkuu.
Nimejaribu kuonana na makamu wa rais kwa njia zote. Nimepiga simu ofisini mwake kila siku na msaidizi wake hunuambia kila mara kwamba hana nafasi kwa sasa. Lakini sikufa moyo, niliamua kwamba lazima nitamuona.


Wiki iliyopita, msaidizi wake alinijulisha kwamba tutapata nafasi ya kuhojiana na makamu wa rais jumanne tarehe 23 mwezi wa Machi saa tatu unusu asubuhi. Nilifurahi sana, Annette na Winston walitabasamu kwa furaha tele.


Siku ilipofika, tulijitayarisha vyema kabisa. Maswali tutauliza, kamera tukaiangalia kama iko sawa, kila kitu tulichobaini kuwa ni muhimu tulichunguza. Tukielekea kumouna makamu wa rais, simu ililia na msaidizi wake akatujulisha kwamba mahojiano yamegeuzwa kua saa kumi siku hiyo. Saa kumi ilipofika tulikuwa ofisini mwake. Chumba chenyewe kilikuwa kimeimarika sana. Lakini tulikosa kumuona siku hiyo maanake alikuwa hajatoka bunge bado. Tuliambiwa kwamba tutaelezwa kesho wakati ambayo atapatikana.
Tulirudi hotelini na huzuni sana. Siku ifuatayo nilipiga simu ofisini mwake kila wakati. Niliambiwa ameingia bunge tena. Ilipofika saa kumi, nilikua nimekufa moyo, ilikua imebaki siku hiyo tu kuhojiana na yeye kwa sababu Annette na Winston walikua wanarudi nyumbani siku ya Alhamisi. Nilikua na huzuni mwingi huku nikijaribu kufikiria njia zingine na kupata kuonana na makamu wa rais.


Mara simu ililia. Msaidizi wa makamu wa rais alikua kwa simu akiniambia nifike kwa ofisi mara moja saa hio. Hoteli ilikua kama dakika thelathini kutoka ofisi ya makamu wa rais. Msaidizi wake alisema niwe hapo kwa dakika kumi. Niliambia Annette na Winston, "Twendeni saa hii, TWENDENI".



Tuliingia teksi na kumwambia dereva aharakishe. Lakini njiani tukapata msongamano wa magari. Kulikuwa kuna nyesha na hatukuweza kutoka kwa gari. Niliuliza dereva kama angeweza kupeleka kwa bara bara iliyo kando yetu ya magari zilizokua zinaenda njia mbadala na sisi. Aliniangalia ni kama nimepagawa, huku Annette anamwambia afanye hivyo. Winston mwishowe akasema tutoke na tukimbie mpaka huko. Tulitoka na kuanza kukimbia ni kama sisi ni wenda wazimu. Lakini hatukujali manake ilikua muhimu sana tumuone makamu wa rais.
Tulifika kwa ofisi yake tumelowa maji, tukihema sana. Lakini tulikua na furaha tele kupata nafasi hii. Mahojiano yalikua mazuri na tulimshukuru makamu wa rais kwa nafasi hio.

Skriv en kommentar