JUMATATU FEBRUARI 22
Changamoto kuu tulilolipata katika mji wa Wamunyu ni ukosefu wa nguvu za umeme. Kamera yetu ilihitaji moto. Ilibidi tutafute jenereta ili kuitia moto kamera yetu.
Katika mji huo kulikua na soko. Mkulimia mmoja aliku amesimama na mbuzi na ng'ombe zake. Tulipata mahali pakuweka mitambo yetu alafu tukazuru mji huo. Watu walituangalia sana, wengine wakituita "MZUNGU" na wengine wakisema ‘MAMBO'.
Mara tukasikia mtu akipiga kelele akisema "MWAMERICA, wewe MWAMERICA". Mtu mlevi alitukujia akiyumba yumba. Akasimama na kutupa mkono wake to msalimie "Habari wamerica, karibuni wamunyu". Tulishangazwa sana lakini tukamsalimia hata hivyo. Tuliongea na yeye kidogo alafu tukaendelea kutembea.
Mwanamme huyo alitufuata kila mahali tulipoenda. Tulijaribu sana kumfukuza, na kumtoroka lakini alikua yuatupata tu. Bado aliku anatuita wamerica na akaanza kubadili nia yake kwetu. Alianza kutuita na ukali. Mwishoe alinikaribia kwa maskio na kusema " wewe mwanaume, Bwana America. Naongea na wewe". Tulipoteza hisia za usalama wakati huo.
Joshua aliku upande mwengine mwa bara bara. Alikua anacheza bao na marafiki zake. Rose alijaribu kumwambia mwanamme huyo awachane nasi lakini akamjibu Rose "Siongei na wewe, naongea na Bwana America." Kitu cha kuchekesha ni kwamba alikua na bendera ndogo ya America ambayo alianza kupepea akisema "Ameeeriiican, Ameeerrriccan!"
Joshua alitokea na akaongea na mtu huyo alafu akaondoka. Nilimwangalia Joshua nikijiuliza nini alichomwambia ndio mtu huyo ili aondoke.
Siku chache baada ya leo tutasafiri kuenda Mombasa ambapo Joshua hufanya kazi. Ni safari ambayo hufanya mara moja kwa mwaka.

Skriv en kommentar